KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.
Dhamira
hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Papa huyo kutaka kulifanya Kanisa
Katoliki liwe rafiki zaidi na kuendana matakwa ya walio wengi.
Akizungumza
kuhusu mabadiliko hayo, Papa alisema si haki kwa wenzi kuishi muda
mrefu ‘wakikandamizwa na wingu la shaka’ kuhusu uhalali wa ndoa zao.
Ikumbukwe
kwamba ni msimamo wa Papa kumkatalia Mfalme Henry the VIII wa Uingereza
kumtaliki mkewe Catherine wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha
England ijitenge na Rome na kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England
huku mfalme akiwa mlinzi wa Imani wa kanisa hilo.
Mabadiliko
makuu matatu aliyotangaza Papa jana ni kuondoa mchakato wa mapitio
ya mara ya pili wa uamuzi wa kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa
kabla ya ndoa kuvunjwa.
Mengine
ni kuwapatia maaskofu uwezo wa kuharakisha na kuvunja ndoa wenzi
wanapoamua wenyewe katika mazingira fulani kama vile ukatili katika ndoa
au uasherati na mchakato huo wa talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa
ada ndogo kwa ajili ya gharama za utawala.
Kabla
ya sheria hiyo, Wakatoliki waliotaka talaka walihitaji kibali kutoka
kwa mahakama mbili za kanisa, wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa
rufaa bado zinaruhusiwa.
Kabla
ya sheria hiyo, wanandoa wa Wakatoliki wanaotalikiana bila idhini ya
kanisa na kuolewa upya walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa
kupokea komunio.
Lakini kwa mujibu wa utaratibu mpya, wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi wa kanisa hilo.
Mwaka
jana Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa hilo kuboresha na
kurekebisha taratibu hizo kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza
gharama.
Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili zinazoitwa ‘motu proprio’, neno la kilatini lililobuniwa na Papa mwenyewe.
Taratibu
hizo zitakuwa rasmi kama sehemu ya sheria za kanisa (canon law) ifikapo
Desemba 8 mwaka huu wakati Papa atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee
ambao kwa kawaida huhusishwa na msamaha.
0 comments:
Chapisha Maoni