Mwenyekiti Taifa wa chama cha Tanzania Labour Party TLP, na mgombea Ubunge jimbo la Vunjo Augustino Mrema, amelalamikia kuwa anafanyiwa siasa chafu na wapinzani wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jimboni Vunjo, Mrema amepeleka lawama moja kwa
moja kwa viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, kwa
kumchafua kwa matusi kwenye kampeni pamoja na kufanyiwa ubaguzi.
“Siwalaumu
wanachama wa CHADEMA, viongozi wao ndio wenye fujo na mimi, sasa
najiuliza tatizo ni nini ,uzee wangu? kama ndio hivyo wawaachie
wananchi, kama kuumwa mbona tangu 1984 naugua kisukari, kwa nini
wananitendea haya?”
Katika
‘line’ nyingine, Mzee Mrema amedai bado ana imani na wananchi wa vunjo
watampigia kura ili awaongoze kwa mika mingine mitano.
0 comments:
Chapisha Maoni