Mchezo huo uliopigwa katika jiji la Liverpool ndani ya uwanja Goodison Park umemalizika kwa Chelsea kuambulia kipigo kingine kwa kufungwa 3-1.
Magoli matatu ya mshambuliaji Naismith yametosha kuipa Everton ushindi mzito dhidi ya vijana wa Jose Mourinho.
Naismith alianza kufunga katika dakika ya 17, dakika 5 baadae akaongeza la pili kabla ya Matic hajaifungia Chelsea goli la kufutia machozi.
Dakika 8 kabla ya mchezo kumalizika Naismith akashindilia msumari wa mwisho na kuipa ushindi wa 3-1 Everton
0 comments:
Chapisha Maoni