Kuwa na ndoto kubwa ni kitu kizuri sana,
lakini juhudi za jinsi gani tutatimiza ndoto zetu sio sawa kwa watu
wote, wengine wanaamini kupiga kazi mpaka mpale juhudi za kazi zao
zitakapowalipa na kuna wengine wanaoamini kuwekeza kwenye njia tofauti…
Gloria Sule ni dada ambaye alikuwa na ndoto kubwa za kuja kuwa mwigizaji maarufu Nollywood Nigeria na alikuwa yupo tayari kufanya kitu chochote kile kutimiza ndoto zake… akiwa kwenye harakati za kutimiza ndoto hiyo Gloria alikutana na mganga Francis Kalu ambaye alimuambia kama akimpatia Naira milioni 2.1 pesa yenye thamani ya Milioni 22, 856,492 kwa Tanzania basi atazitimiza ndoto zake!
Baada ya kutoa hiyo pesa, mganga huyo
alimwambia ili kukamilisha dawa ya mvuto ya ustaa itambidi atimize
baadhi ya masharti ya mganga huyo ikiwa kuonga nae ili kuruhusu dawa
aliompa kufanya kazi… lakini baada ya kufanya yote hayo Gloria hakuona kitu chochote kikitokea na ndipo alipoamua kwenda polisi kumshitki mganga huyo.
Mganga alikamatwa na kupelekwa polisi, kesi ikafika mpaka kwenye Mahakama ya Ejigbo Magistrate’s court jijini Lagos walivyokuwa huko Francis Kalu akasema hana kesi ya kujbu kwani dada huyo alitaka mwenyewe kuchezewa… kesi hiyo imeairishwa na imepangwa kusikilizwa tena September 21 wezi huu.
Mganga huyo anashitakiwa kwa kosa la uwizi, na utapeli kwa mujbu wa Sheria ya Makosa ya Jinai ya Nigeria.
0 comments:
Chapisha Maoni