test

Jumapili, 13 Septemba 2015

Magufuli Azidi Kuchanja Mbuga.....Maelfu ya Wananchi Wahudhuria Mikutano yake Simiyu



Mgombea Urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa mji wa Lamadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi hao wanaondokana na tatizo sugu la upatikanaji maji.
 Mgombea Ubunge jimbo la Busega Dk. Raphael chegeni akihutubia wakazi wa mji wa maji kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizoongozwa na mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani (kushoto) ,wakipena mikono na Mgombea ubunge wa jimbo la Busega kupitia CCM Dk. Raphael Chegeni wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika mji wa Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa bariadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa CCM Saba saba.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Maetu kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa atatatua tatizo kubwa la maji kwa kuchukua maji kutoka ziwa Victoria.
 Hivi ndivyo meatu ilibyofurika.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr. Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Meatu.
 Wasanii wa Original Komedi wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya stendi Meatu.
 Meatu
 Wakazi wa Ikindilo wakimsikiliza mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wakazi wa Bariadi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM saba saba.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni