Ratiba za kampeni za wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaonekana kuchuana vikali, Edward Lowassa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeibua mgongano.
Hali
hiyo imelalamikiwa na CCM ambayo imeitupia lawama Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) kwamba imeshirikiana na Chadema kupanga njama hizo.
Kufuatia hali hiyo, jana Nec iliingilia kati na kuitisha kikao cha kupitia upya ratiba za kampeni za vyama.
Kampeni
za vyama ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajia
kufanyika Oktoba 25, zilianza rasmi Agosti 22, mwaka huu baada ya Nec
kufanya uteuzi wa wagombea.
Kwa
mujibu wa taratibu na sheria, kabla ya kampeni kuanza vyama vya siasa
vinavyoshiriki uchaguzi hutakiwa kuwasilisha ratiba zao Nec na baadaye
tume hiyo hupanga ratiba ya nchi nzima kujumuisha vyama vyote.
Hata
hivyo, kampeni za wagombea wa vyama hivyo mikoani zinaonyesha kuwa
wamekuwa wakifuatiliana hususani Lowassa kwenda maeneo ambayo Magufuli
anatoka kujinadi kwa wapigakura.
Lowassa
alianza ziara yake mikoani Agosti 30, mwaka huu katika mkoa wa Iringa
ambako alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mufindi, Kilolo na
Iringa mjini.
Baadaye
aliendelea na ziara yake katika mkoa wa Njombe ambako alifanya mikutano
ya kampeni katika majimbo ya Makambako na Njombe mjini.
Kwa
upande wake, Dk. Magufuli alitangulia kufanya ziara katika mkoa wa
Njombe na kufanya mikutano katika jimbo la Njombe mjini ambako Lowassa
alifanyie mkutano eneo hilo hilo.
Majimbo mengine aliyotembelea ni Makete mjini na Wanging’ombe.
Mkoa wa Ruvuma
Dk.
Magufuli alitangulia kufanya ziara kwa kufanya mikutano katika majimbo
ya Madaba, Nyasa, Mbinga mjini, Peramiho na kufunga pazia Songea mjini
katika uwanja wa Majimaji.
Kwa upande wake, Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika jimbo la Madaba, Songea mjini na Tunduru.
Mkoa wa Katavi
Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Nkasi, Mpanda mjini na Namanyele.
Kwa
upande wake, Magufuli ambaye alikuwa wa kwanza kuwasili mkoani humo,
alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mpanda vijijini na Mpanda
mjini.
Mkoa wa Rukwa
Dk. Magufuli alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Milele, Nkasi, Kalambo na Kwela.
Mkoa wa Morogoro
Dk. Magufuli alifanya mkutano wa kwanza wa kampeni jimbo la Mahenge, Malinyi, Ifakara na Morogoro mjini.
Walivyogongana Njombe,Iringa
Magufuli aliingia Njombe na kufanya mikutano katika jimbo la Njombe Mjini, Makete Mjini na Wang’ing’ombe.
Lowassa
alianza ziara yake mikoani Agosti 30. Akatua Iringa katika majimbo ya
Mufindi, Kilolo na Iringa Mjini. Kisha akatua Njombe alikotoka Magufuli
na kuhutubia Makambako na Njombe mjini.
Ruvuma
Dk. Magufuli aliingia Ruvuma na kufanya mikutano Madaba, Nyasa, Mbinga Mjini, Peramiho na kumalizia Songea Mjini.
Lowassa
naye akatua na kufanya mikutano ya kampeni alikopita Magufuli katika
majimbo ya Madaba, Songea Mjini na kisha akafanya hivyo Tunduru.
Katavi
Magufuli aifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mpanda Vijijini na Mpanda Mjini.
Siku chache baadaye, Lowassa alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Nkasi, Mpanda Mjini na Namanyele.
Rukwa
Dk.
Magufuli alifanya mikutano ya kampeni katika majimbo ya Mlele, Nkasi,
Kalambo na Kwela. Hata hivyo, Lowassa hajafika katika majimbo ya mkoa
huo.
Morogoro
Mwishoni
mwa wiki, Dk. Magufuli alifanya mikutano ya kampeni mkoani Morogoro
katika majimbo ya Mahenge, Malinyi, Ifakara na Morogoro Mjini.
Ratiba ya Lowassa inaonyesha kuwa naye atakuwa Morogoro leo kuanza mikutano yake ya kampeni mkoani humo.
Kutokana na ratiba hiyo kugonganisha wagombea hao, baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM wamekuwa wakilalamikia suala hilo.
Kauli ya NEC
Mkurugenzi
wa Nec, Ramadhani Kailima, alipotafutwa ili kueleza kwa nini ratiba ya
kampeni ya wagombea urais wa CCM na Chadema inagongana, alisema jana
tume ilikutana na vyama vya siasa kwa ajili ya kupitia upya ratiba ya
kampeni iliyotolewa awali.
“Naongoza kikao cha kamati ya vyama kupitia ratiba ya kampeni za kiti cha rais na makamu wa rais,” alisema.
Kailima alisema Nec haipangi ratiba isipokuwa vyama vyenyewe hufanya hivyo chini ya uratibu wa tume.
“Leo (jana) tuko na vyama wanapitia ratiba, anayepanga ratiba siyo Nec ni wao wenyewe chini ya uratibu wa tume.
"Leo jioni (jana) tutakuwa tumemaliza kikao na vyama vyenye wagombea urais tutaweka (kwenye tovuti) ratiba mpya,” alisema.
Malalamiko ya CCM
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, alisema wamebaini kuwa Nec,
ilikula njama na Chadema katika kutengeneza ratiba za wagombea urais kwa
kuwa walishinikiza ratiba ya CCM kuwafikia mapema.
“Tumegundua
Chadema walitaka ratiba yetu itangulie, waliwasumbua wasaidizi wangu
wakieleza sisi (CCM) pekee tumebaki hatujapeleka ratiba kumbe siyo
kweli, na Chadema walitengeneza ratiba kwa kuangalia ya kwetu,” alisema.
Luhavi
alisema kwa mazingira hayo ratiba inayofanyiwa kazi awali ni
iliyotangulia kufika Nec na baada ya kuligundua hilo chama kimeweka
mkakati na mabadiliko yataonekana hivi karibuni.
NEC Yajibu
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Nec, Kailima, alipoulizwa kuhusu tuhuma za CCM
alijibu kwa kifupi kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kuwa:
“Nadhani waliosema wana nafasi nzuri ya kusema, mini siyo msemaji wao, waulize wao (CCM) waliosema.”
CHADEMA: CCM wametufuata Mikoani
Mkuu
wa Kitengo cha Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema ratiba yao ya
kampeni waliipanga mapema kwa kuzingatia kanda, hivyo inawezekana CCM
ndio wamewafuata katika mikoa waliokuwa wamepanga kwenye ratiba hiyo.
“Hata
kama Chadema watatangulia katika mkoa au jimbo fulani kufanya mkutano
wa kampeni na baadaye ikafuata CCM, eneo hilo hilo haiwezi kuaithiri
Ukawa kwa sababu wananchi wameshaamua kuwa na mabadiliko,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni