Wananchi
wameeleza kuchoshwa na rushwa ambayo wameitaja kama saratani
inayodumaza maendeleo ya nchi na kutaka rais ajaye apambana na tatizo
hilo kwa dhati bila woga .
Wakizungumza na ITV katika mwendelezo wa kampeni za kumnadi mgombea
wa kiti cha urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli wananchi hao wa
mji wa Meatu wamesema kukosekana kwa huduma nyingi za kijamii ili
kumrahisishia maisha mtanzania wa kawaida kunasababishwa na vitendo vya
rushwa vinavyofanywa na watendaji wa serikali jambo linaloonekana kama
utaratibu wa kawaida hivyo kumtaka rais ajaye kukomesha vitendo vya
rushwa kwa vitendo katika sekta zote za utoaji wa huduma.
Mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli kwa
upande wake ameeleza kuchukizwa na vitendo vya rushwa na ufisadi
kunakosababisha huduma kutomfikia mwananchi wa kawaida na kwamba
litakuwa suala la kipaumbele kupambana nalo na kuwataka watendaji
wajipange kutoa huduma bora na kutatua kero za wananchi.
Aidha Dr.Magufuli ameongeza kuwa serikali ya awamu ijayo endapo
atapata ridhaa mbali na kutaka uchumi wa nchi uendeshwe kwa kutegemea
viwanda pia atatilia mkazo katika sekta ya uvuvi na kilimo hususani cha
mazao yanayowaingizia kipato kikubwa wananchi ili kukuza kipato cha kaya
na taifa lakini pia kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
Mh.Luaga Mpina akiwawakilisha wananchi wake amemuoba Dr. Magufuli
atakapoingia ikulu kusaidia kutatua kero kubwa inayowakumba wananchi wa
meatu ambao kwa kiasi kikubwa ni wafugaji na wakulima kuwatengea maeneo
ya kilimo na ufugaji ili kupunguza migogoro iliyopo.
Dkt.Magufuli atahitimisha ziara ya kunadi ilani ya ccm katika
wilaya za mkaoa wa simiyu na kuingia mkoani tabora kuhutubia mkutano wa
hadhara wa kuomba ridhaa kwa watanzania waishio mkoani Tabora.
0 comments:
Chapisha Maoni