Chama
cha CUF wilayani Ikungi kimekilalamikia chama cha demokrasia na
maendele Chadema mkoa wa Singida kwa kuweka wagombea udiwani wote wa
wilaya hiyo na kukiuka utaratibu wa UKAWA wa kusimamisha mgombea anaye
kubalika bila taarifa yeyote.
Akiongea katika kikao cha viongozi wa CUF na wagombea udiwani wa
chama hicho katibu wa CUF wilaya ya Ikungu Bwana Selemani Ntandu amesema
tokea tarehe kumina tatu mwezi huu baada ya vyama vya siasa kutia saini
makubaliano ya mgawano katika kata yeye mpaka sasa haja pata taarifa
yeyote na kushutukia Chadema wamesha chukuwa fomu za kugombea.
Baada ya kubaini hivyo mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ikungi na
mjumbe wa baraza kuu la uongozi wa CUF taifa Bwana Athumani Hengu
amesema CUF wilayani Ikungi wamefanikiwa kuungwa mkono katika kata
nyingi na kupata wawakilishi wa udiwani karibu kata zote.
ITV na Radio One ilifanya juhudi za kumtafuta mwenyekiti wa Chadema
mkoa wa Singida Bwana Shabani Hamisi Limu nayeye amesema CUF wilayani
Ikungi hawakuwa wamejiandaa kwenye uchaguzi wa udiwani na kutokana na
hali hiyo wao Chadema iliwalazimu madiwani wao wote kuchukuwa fomu za
kugombea, kwa hiyo malalamiko yao siyo ya msingi.
0 comments:
Chapisha Maoni