Mwanasheria huyo aliywahi kukalia kitu cha uwaziri wa mambo ya
ndani ya nchi alifikishwa mahakamani hapo akitokea katika gereza la
Segerea baada ya jana mahakaam kuamuru maafisa wake kufanya uhakiki wa
dhamana za mtuhumiwa huyo.
Mbele ya hakimu mkuu mkazi wa mahakama hiyo Riwandere Lema
mwanasheria wa serikali Wankyo Simon ameithibitisha mahakama kuwa
wadhani Wilfred Mush na Maadra Erenest wanasifa halali za kumdhani
mtuhumiwa na kutakiwa kusaini hati ya shilingi milioni moja kila mmoja
na ilipotimu majira ya saa 3.45 Lawrence Masha akawa nje kwa dhamana.
Katika kesi ya msingi Masha anatuhumiwa kutumia lugha ya matusi
kinyume na kifungu cha sheria ya makosa ya jinai matusi amabyo anadaiwa
kuyatoa katika kituo cha polisi cha Osterbay Dar es Salaam mapema Agost
24 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatarajiwa tena Sept 7 mwaka huu.
Katika hatua nyingine mahakama hiyo imeahilisha kesi inayomkabili
aliyekuwa na mwenyekiti wa CUF na wenzake mpaka Septemba 28/30 baada ya
watuhumiwa wawili kushindwa kufika mahakamani hapo.
Katika kesi ya msingi Lipumba na wenzake 30 wanakabiliwa na
mashitaka matatu ambapo inadaiwa Januari 27 mwaka huu eneo la Temeke kwa
pamoja waliitenda kosa la kufanya mkusanyiko kinyume na taratibu huku
shitaka la pili wakidaiwa kufanya mkusanyiko usiohalali kwa kufanya
maandamano kwenda Mbagala Zakiem.
Na shitaka la tatu wakidaiwa kugoma kutii tangazo la polisi lililowataka wasiaandamane na kutokufanya mkusanyiko usiohalali.
0 comments:
Chapisha Maoni