Rais Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi
wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka
huu tukio liloenda sanjari na uzinduzi wa ilani ya chama hicho pamoja na
kuwatambulisha mgombea urais na mgombea mwenza wake ambapo amesema kwa
vigezo alivyonavyo Magufuli juu ya utendaji wake hodari anaamini
watanzania watampa kura za kutosha.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na marais wastaafu akiwemo Alhaji Hassan
Mwinyi na Mh Benjamin William Mkapa na baadhi ya mawaziri wakuu wastaafu
ambapo wakihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga
vyake marais hao wastaafu mbali na kummwagia sifa kedekede mgombea urais
Mh John Magufuli na mgombea mwenza wake amewahakikishia watanzania kuwa
kati ya wagombea nane waliopitishwa na NEC team bora ni Mh Magufuli na
Mh Samia Suluhu.
Kwa upande wake rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amesema kwa historia ya Zanzibar na
Tanganyika wanzanzibar watamuunga mkono Mh Magufuli kwa nguvu zote huku
akiwataka watanzania wote waendelee kuwaelimisha wengine ili wasifanye
mchezo wala wasijaribu kwani dola siku zote haijaribiwi.
Waziri mkuu mstaafu Mh Joseph Sinde Warioba akapata nafasi ya
kuhutubia umati huo wa watu ambapo ameuleza kuwa mkutano mkuu wa CCM
ulisikiliza maombi na kilio cha wana CCM ambao walitaka mgombea
mwadilifu na mchapakazi na Mh Magufuli maeneo yote aliyopewa aliyamudu
na matunda yake yameonekana.
Funga kazi ikaishia kwa mgombea urais Mh John Pombe Magufuli na
mgombea mwenza wake Mh Samia Suluhu ambaye ameahidi pindi tu atakapopata
ridhaa ya watanzania ataunda mahakama maalum ya kushughulikia mafisadi
na wezi kwani ndio walioifikisha nchi hapa ilipo na atasimamia utawala
bora ikiwa ni pamoja na kuheshimu mawazo ya vyama vingine yenye kujenga
nchi.
Uzinduzi huo umepambwa na burudani mbalimbali ambazo wakati wote
ziwafanya wahudhuriaji hao wasichoke zikiwemo nyimbo maridhawa za chama
hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni