WAZIRI
Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye amechukua fomu za kuomba kuwania urais
kupitia CCM, amesema atakuwa tayari kumuunga mgombea yeyote
atakayepitishwa na chama chake. Alisema akikosa yeye atafurahi
akiteuliwa Profesa Mark Mwandosya.
Akitoa
salamu kwa wanachama wa chama hicho waliofika kumdhamini katika Wilaya
za Mbozi, Mbeya vijijini na Mbeya Mjini ambapo zaidi ya wanachama
6,000 walimdhamini, wakati wanaotakiwa ni 30.
Akisalimia
wananchi wa Mbozi akitokea Rukwa, alisema katika Kanda ya Nyanda za
Juu Kusini, wamepata heshima ya kuwa na wagombea wawili ikiwa ni yeye
na Profesa Mwandosya, hivyo akishinda yeye itakuwa ni mipango ya Mungu
na akishinda Mwandosya pia atafurahi kwa kuwa itakuwa ni heshima kwa
wananchi wa kanda hiyo.
Alisema
Chama hicho ili kishinde kinahitaji upendo na mshikamano. Alisisitiza
kuwa hakuna maana ya kushambuliana na kuchafuana kutokana na kuwa
waliochukua fomu wote ni wana-CCM na hadi sasa hakuna mwenye uhakika
wa kushinda kutokana na siri hiyo Mungu pekee kuijua.
"Anayejua
hadi sasa kuwa Rais wa Tano wa Tanzania ni nani ni Mungu pekee na
hivyo hakuna maana ya kushambuliana kwani tunaweza kufika mwisho wa
safari wakiwa vipande vipande na hivyo kuzalisha makundi makubwa ndani
ya chama ambayo yatakipa shida chama kupata ushindi wa kishindo," alisema.
Alitaka
wagombea kuacha kujiaminisha ushindi kwa jambo ambalo alisema
haliwezekani kwa wao kuwa na uhakika wa jambo hilo kutokana na ukweli
kuwa anayejua mshindi ni Mungu peke yake.
"Wako
watu hadi sasa utawasikia wanasema kuwa lazima mimi niwe
mimi,lazima niwe mimi jambo ambalo si la kweli kutokana na kuwa
anayejua hayo ni Mungu peke yake na hivyo wanachotakiwa kujua kwa
sasa ni kuwa kazi yao ni kueleza mikakati yao badala ya kujipa uhakika
wa kushinda," alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni