JAJI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhani (70) ambaye kwa sasa ni Rais wa Mahakama ya Afrika, amepandisha joto la urais ndani ya CCM, baada ya jana kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mara baada ya kuchukua fomu, Jaji Ramadhani ambaye pia ni mwanajeshi
aliyestaafu akiwa na cheo cha Brigedia Jenerali, kiongozi wa dini akiwa
Mchungaji wa Kanisa Anglikana na mwanamichezo mahiri, alisema
amejitokeza kwa kuwa ana uwezo wa kutosha katika kuongoza nchi.
Pia ameahidi kuyaangalia mapendekezo ya wananchi yaliyoachwa kwenye
Katiba Inayopendekezwa iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi kwani
katiba ni ya wananchi.
“Sina makeke ndiyo maana nimeongozana na watu wachache kuja kuchukua
fomu, siku zote chema chajiuza,” alisema.
Alisema yeye ni mtu safi na hajawahi kutajwa mahali popote kuhusika na ufisadi kutokana na kuwa na mapenzi wa kuitumikia nchi yake na atahakikisha anashughulika na tatizo la rushwa na ufisadi katika nchi.
Alisema yeye ni mtu safi na hajawahi kutajwa mahali popote kuhusika na ufisadi kutokana na kuwa na mapenzi wa kuitumikia nchi yake na atahakikisha anashughulika na tatizo la rushwa na ufisadi katika nchi.
Akiwa ameongozana na mkewe, Saada Mbarouk Ramadhani ambaye ni
mwanajeshi wa ngazi ya juu mwenye cheo cha Luteni Kanali, alisema ana
uzoefu wa kutosha ndio maana anaomba dhamana ya chama na wananchi ili
aweze kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
“Nina vigezo vya kutosha na nia uwezo najiamini, nataka nipate nafasi
ya kuteuliwa na chama na baadaye niwe kiongozi mkuu wa nchi ili kwa
pamoja tuijenge nchi yetu,” alisema Jaji mstaafu Ramadhani, tofauti na
wagombea wengine zaidi ya 35 waliomtangulia kuchukua fomu CCM,
hakujieleza, bali alitaka kuulizwa tu maswali na waandishi wa habari.
“Mimi sikuitisha kikao cha kutangaza nia ninataka waandishi waniulize
maswali tu,” alisema.
Alipoulizwa kama anaona kuna mgombea yeyote ambaye ni tishio kwake alisema, yeye ni Brigedia Jenerali hawezi kuogopa chochote.
Alipoulizwa kama anaona kuna mgombea yeyote ambaye ni tishio kwake alisema, yeye ni Brigedia Jenerali hawezi kuogopa chochote.
Pia alipohojiwa akiwa rais atawezaje kuondoa tatizo la rushwa na
ufisadi na hata tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, alisema
matatizo hayo yote yatatafutiwa dawa mapema kwani hata alipokuwa Jaji
Mkuu alizunguka mikoa 15 ambapo alikutana na wakuu wa mikoa na wilaya na
walizungumzia suala hilo.
“Suala la rushwa na ufisadi ni mtoto pacha, sheria zipo ni
utekelezaji tu unaotakiwa,” alisema.
Alisema tatizo la mauaji ya walemavu wa ngozi Serikali inajitahidi na wale waliohusika wamefikishwa mahakamani wengine wamehukumiwa adhabu ya kifo na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa adhabu hizo.
Alisema tatizo la mauaji ya walemavu wa ngozi Serikali inajitahidi na wale waliohusika wamefikishwa mahakamani wengine wamehukumiwa adhabu ya kifo na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa adhabu hizo.
Alisema elimu zaidi inatakiwa kutolewa ili wananchi wafahamu viungo
vya albino havileti utajiri. Pia alipohojiwa kwamba, wakati akiwa kama
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba kuna mapendekezo ya
wananchi yaliachwa, atafanyaje akipata nafasi ya kuongoza nchi?
Alijibu kwa kusema Katiba ni ya wananchi si ya kwake na atasikiliza
matakwa ya wananchi kama wakihitaji yarudishwe basi yatarudishwa.
Alipohojiwa amekuwa mwanachama wa CCM tangu lini alisema ameingia kwenye
siasa mwaka 1969.
Alisema alikuwa mwanachama wa Umoja wa Vijana wa Tanu tangu Agosti,
mwaka 1969 wakati huo akiwa mwanafunzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Akiwa chuoni wakati akikaribia kumaliza shahada yake akatuma maombi
ya kujiunga na jeshi na na akaulizwa kama ni mwanachama wa Tanu akasema
ni mwanachama wa Vijana wa Tanu akaambiwa lazima awe mwanachama wa Tanu
ndipo ajiunge na jeshi.
Alisema alikwenda kufuatilia kadi ya Tanu na alifanikiwa kuipata na
aliendelea kuwa na mwanachama wa CCM hadi mwaka 1992 wakati mfumo wa
vyama vingi vya siasa ulipoanza na Katiba kukataza majaji kuwa wanachama
wa vyama vya siasa.
Jaji mstaafu Ramadhani alisema alipostaafu ujaji mwaka 2011 alirudi
tena na kuwa mwanachama wa CCM. Pia alipopata tu shahada ya chuo kikuu
alijiunga na jeshi moja kwa moja na mwaka 1971 aliteuliwa kuwa Luteni
Usu kwa kuwa alikaa makao makuu ya jeshi na ilipoanzishwa Brigedi ya
Faru mkoani Tabora.
Alisema Rais wa Zanzibar wakati huo, Mzee Aboud Jumbe alimuita arudi
Zanzibar ili awe Mwanasheria Mkuu lakini alitaka kujifunza kwanza kabla
ya kushika nafasi hiyo.
Mwaka 1978 akawa Naibu Jaji Mkuu wa Zanzibar na wakati wa vita baina
ya Tanzania na Uganda alikwenda vitani na alirejea Zanzibar mwishoni mwa
mwaka 1979 na ndipo akateuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Alipotoka Zanzibar aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Nchini
kwa miaka 20, baadaye Jaji Mkuu miaka mitatu na nusu akastaafu na sasa
ni Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika.
Historia yake
Jaji Agustino Ramadhani alizaliwa Desemba 28, 1945 mjini Unguja, Zanzibar akiwa mtoto wa pili kati ya wanane waliozaliwa kwa wazazi wake.
Jaji Agustino Ramadhani alizaliwa Desemba 28, 1945 mjini Unguja, Zanzibar akiwa mtoto wa pili kati ya wanane waliozaliwa kwa wazazi wake.
Baba yake ni Mathew Douglas Ramadhani, raia wa Zanzibar aliyefariki
dunia mwaka 1962 na mama yake, Bridget Ramadhani alifariki dunia mapema
mwaka huu. Watu wengi hushangaa kuona au kusikia ana majina mawili ya
dini tofauti.
Agustino (jina la Kikristo) na Ramadhani (jina la Kiislamu). Lakini
ukweli wa mambo ni kuwa yeye ni Mkristo wa madhehebu ya Anglikana na ni
mchungaji wa kanisa hilo.
Elimu ya msingi aliianzia wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma katika
Shule ya Msingi Mpwapwa mwaka 1952 -1953 darasa la kwanza na la pili.
Baadaye alihamia mkoani Tabora na kusoma darasa la tatu na la nne
katika Shule ya Mingi “Town School” mwaka 1954 – 1956. Mwaka 1957 – 1958
alisoma darasa la sita na la saba katika Shule ya Msingi Kazel Hill
(sasa inaitwa Shule ya Msingi Itetemia), kabla ya kurudi Mpwapwa ambako
alikamilisha darasa la nane mwaka 1959.
Aijiunga na Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora mwaka 1960-1965 kwa
ajili ya elimu ya kidato cha kwanza na nne pamoja na elimu ya kidato
cha tano na sita.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alipata fursa ya kujiunga katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akianza kusomea Sheria. Shahada hii nyeti
aliisoma kuanzia mwaka 1966 hadi alipohitimu Machi 1970 na baada ya
kuhitimu alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria na
aliajiriwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kufanya
kazi za uanasheria.
Kwa mtu mwenye shahada ya chuo kikuu enzi za miaka ya 1970, kupanda
vyeo kilikuwa kitu cha lazima. Jeshi halikuwa na wasomi wengi kama
ilivyokuwa katika sekta nyingine na kila aliyekuwa na elimu kubwa
alikuwa mtu muhimu.
Ndiyo maana haikushangaza kwamba mwaka 1971 tayari alikuwa Luteni
(nyota mbili) akiwa kambi ya Mgulani na miaka sita baadaye akahamishiwa
Brigedi ya Faru mkoani Tabora wakati huo akiwa tayari ni Meja.
Kutoka hapo, alifanya kazi jeshi na uraiani kwa vipindi tofauti hadi
alipostaafu na sasa kujiona ameshakomaa katika nyanja nyingi, hivyo yuko
tayari kuvaa viatu vya Rais wa Awamu ya Nne anayemaliza muda wake, Rais
Jakaya Kikwete.
Anakuwa Mzanzibari wa tatu kujitosa Urais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania mwaka huu, wengine wakiwa Mtoto wa Mwasisi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Balozi Ali Karume na mwanadiplomasia aliyewahi kuwa
Waziri wa Fedha wa Zanzibar na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Tanzania, Amina Salum Ali ambaye kwa sasa ni Balozi wa
Umoja wa Afrika (AU) huko Marekani.
0 comments:
Chapisha Maoni