test

Ijumaa, 12 Juni 2015

Urais 2015: Pinda achukua fomu, apanga kukuza uchumi>>>




Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akiwa ameshika fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kitabu baada ya kuwasili kuwasili kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini Dodoma kuchukuwa fomu za kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda leo amechukua fomu ya kuwania kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, mara baada ya kuchukua fomu  Waziri mkuu Pinda amezungumza na Waandishi wa Habari vipaumbele vyake ikiwa atapitishwa na Chama chake  cha Mapinduzi kugombea Urais katika uchaguzi utakaofanyaika mwezi oktoba mwaka 2015  ambavyo ni kuongeza ukuaji wa uchumi na kuondoa pengo kubwa lililopo kati ya wenye nacho na wasio nacho.

Akizungumzia uzoefu wake katika uongozi amesema  ana uzoefu na mafanikio yote ya Wizara yeye ndiye Kiranja wake.

Hata hivyo, ametilia mkazo kuwa hawezi kuzungumza mambo mengi kwa kuwa hataki kuingilia ilani ya chama chake.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni