Timu ya Taifa ya Brazil
imechinjwa goli 1-0 dhidi ya Colombia katika mechi ya pili ya kundi C ya
michuano ya mataifa ya America kusini, (Copa America) inayoendelea
nchini Chile.
Goli pekee la ushindi la Colombia
kwenye mtanange huo uliochezwa uwanja wa Santiago limefungwa dakika ya
36′ kupitia kwa Jeison Murillo.
Dakika ya 90′ Neymar wa Brazil na Carlos Bacca wa Colombia walioneshwa kadi nyekundu baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.
Kadi hiyo ni aibu kubwa kwa
Neymar kwani haikuwa na ulazima ikizingatiwa yeye ndiye nahodha wa
Brazil na amebeba matumaini ya timu hiyo ambayo bado ina machungu ya
kupigwa 7-1 na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia
lililofanyika mwaka jana kwenye ardhi ya nyumbani kwao.
Tukio lilikuwa hivi: baada ya
mwamuzi raia wa Chile, Enrique Osses kupuliza filimbi ya kumaliza mpira,
Neymar alimpigia mpira kwa makusudi, mpira uliomgonga mgongoni Pablo
Armero wa Colombia na ndipo vurumai ikaanza baina ya wachezaji wa timu
zote mbili.
Wakati fujo hizo za wachezaji
zikiendelea, Carlos Bacca alimsukuma mgongoni Neymar na ndipo mwamuzi
akawaonesha kadi nyekundu ya moja kwa moja wote wawili (Neymar na Carlos
Bocca).
Kwa mara nyingine tena, Radamel Falcao alionesha kiwango cha chini kabla hajatolewa baadaye wakti mchezo unaendelea.
Mechi nyingine ya kundi C itapigwa usiku wa kuamkia kesho kati ya Peru na Venezuela.
0 comments:
Chapisha Maoni