Hivi karibuni ishu ya wanaume wa Rombo kujihusisha na pombe haramu aina ya gongo na kusahau majukumu ya familia zao ilikaa kwenye headlines kwa muda mrefu na hata kufikia kuzungumzwa sana hata bungeni
Matumizi
ya unywaji wa pombe hiyo si tu inanyweka Tanzania kwani leo headlines
zimehamia nchini India baada ya watu 35 kupoteza maisha katika mji wa
Mumbai baada ya kunywa pombe hiyo na wengine kulazwa hospitali.
Hata
hivyo Serikali ya nchi hiyo imeingilia kati baada ya kutaka uchunguzi wa
kina ufanyike huku watu watatu wakishikilia kwa tuhuma hizo.
Unywaji
wa pombe hiyo umeshika kasi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo huku
bei ya kununua imekua iko chini ya dola moja na kufanya idadi ya
wanywaji kuomgezeka huku Mwaka 2011 kuliripotiwa kupoteza maisha kwa
watu 170 kutokana na unywaji wa pombe hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni