Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati) wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya leo Juni 19, 2015 kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mbeya wamevunja rekodi ya udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward
Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi
wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM
Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.
0 comments:
Chapisha Maoni