Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema anaamini kuwa muigizaji
huyo anaweza kuwa kiongozi mzuri japo changamoto inayomkabili ni
kubadilisha mawazo ya watu juu yake hasa kutokana na maisha yake ya
ustaa na mapenzi.
Martin ameiambia Mpekuzi kuwa kinachotakiwa sasa ni kuwabadili watu waanze kumchukulia kama mwanamke anayeweza kuwa kiongozi.
“Watu wengi wametokea kumsupport kwa sababu walikuwa wanamsikia baba
yake akimtaka aingie kwenye siasa, na wengine walikuwa wanamtaka Wema
aingie kwenye siasa,”amesema Martin.
“Lakini ana kazi kubwa ya kuweza kubadilisha watu jinsi
wanavyomchukulia. Kwahiyo anachukulia positive kwa sababu watu aliokuwa
nao wameweza kumsupport. Lakini kabla hatujafika huko sasa tutamuona
kama kiongozi sioo kama msichana wa bongo movie. Tumuamini Wema kama
anaweza kuonyesha tu nia hata asipopata tukumbuke kuonyesha nia tu ni
kupata, kwa sababu ana ndoto kubwa sana anataka kuzifanya,” ameongeza.
Hivi karibuni Wema alitangaza nia ya kuwania ubunge wa viti maalum kwa tiketi cha chama cha mapinduzi mkoani Singida.
Kupitia Instagram aliandika:
Naanza kwa kusema Alhamdulillah kwa kufikia hapa nilipo na
nawashkuru sana wazazi wangu kwa kunileta duniani na kunilea katika
maadili mazuri… Nawashkuru pia kwa kunipa Elimu na kunipa chochote
nilichokitaka but more over kwa kunipa support kubwa katika uamuzi
wowote niliokuwa nimeufanya… Kwanzia kushiriki Miss Tanzania mpaka pale
nilipoamua kujiingiza katika maswala ya sanaa.
Vitabu vya dini vimeandika inapaswa tumshukuru Mungu kwa kila jambo,
liwe zuri au baya… Pale Mungu alipoamua kumchukua Daddy Sepetu wangu
niliumia sana na nikawa nimeona kama maisha yangu yalirudi nyuma kidogo,
maana ilinibidi nianze kuishi maisha ya No More Daddy Sepetu….
Maana
nilikuwaga ni kipenzi cha Daddy wangu cuz I happen to be da last born,
mwenyewe alikuwa akiniita Miss World wake…. Nakumbukaga My Late Daddy
Sepetu alishawahi kuniambia kuwa nijaribu kujiingiza katika politics
since yeye na siasa ilikuwa ni kama uji na mgonjwa… And I remember
nilimwambia ,”Daddy Sepetu NO sitoweza” …
Alikuwa heart broken sana
maana alihisi nikijaribu ntaweza na kilichokuja kumvunja moyo ni
nilipochukua uamuzi wa kufanya International Business na sio hata
Political science au chochote kilichohusu Siasa nilipoenda Chuo
But hakukata tamaa… Akazidi kuniambia naweza na nilizidi kukataa… Daddy Sepetu wangu This is for u…. Leo hii nimejikuta mwenyewe nimefanya uamuzi mzito wa kujiingiza kwenye Siasa na kuona wat it has in store for me… Najua you are looking down on me smiling… Ila tu jua kuwa Your wife ambaye ni my Darling Mother nae pia amechangia kiasi kikubwa sana…
Nawapenda sana wazazi wangu maana wanajua Whats Best for me… Haya
sasa naingia vitani… Na sitokubali Defeat… Tho kuna mengi yanaweza
tokea… Namkabidhi Allah yote…. Na niko tayari kwa chochote… Penye nia
siku zote njia haiwezi kukosekana.
0 comments:
Chapisha Maoni