Linah Sanga amesema taarifa kuhusu uhusiano kati ya Wema Sepetu na aliyekuwa mpenzi wake umemshangaza.
Akiongea kwenye kipindi cha Ala za roho cha Clouds FM, Linah alisema
yeye na mpenzi wake waliachana rasmi miezi miwili iliyopita.
“Hata mimi nasikia kuwa sasa hivi anatoka kimapenzi na Wema Sepetu,”
alisema Linah. “Unajua mtu kama alishawahi kuwa mtu wako lazima upate
mshtuko, kwakweli hata mimi imenishtua sana.
"Kwahiyo mimi namuachia
Mungu, nina imani aliyopanga Mungu binadamu hawezi kupangua. Na pia
nawatakia kila lakheri katika mahusiano yao.
" Sasa hivi nipo busy na kazi
zangu maana mimi sikuzaliwa naye na wala sitozikwa naye. Na mimi kwa
upande wangu nipo poa kabisa.”
0 comments:
Chapisha Maoni