Shilole a.k.a Shishi bybee sasa anaweza kupata usingizi mnono bila mawazo, sababu lile sakata la kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji mwezi uliopita hatimaye limemalizika vizuri.
Sakata hilo lilifika hadi bungeni ambapo Naibu Waziri wa
Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema serikali
ililiagiza Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kufanya naye mahojiano ili
serikali iweze kuchukua hatua.
Muimabaji huyo wa ‘Nakomaa na JIji’ ameelezea furaha yake baada ya kusamehewa na BASATA alipoenda kutoa maelezo.
“Leo nimeenda BASATA kwasababu waliniita juzi, kwahiyo nimeenda
kusikiliza wito wao, tumeongea nashukuru wamenielewa tumeongea
tumeelewana basi hakuna tena kitu ambacho kina tatizo tena hapo
kwasababu wale ni wazazi wanatakiwa kumkanya mtu kama mtoto labda”
Alisema Shishi bybee
“Tumeelezana pale nini kifanyike nini kisifanyike na kila kitu
ambacho kinahusiana na tasnia ya sanaa. Nimewaelezea situation
ilivyotokea wamenielewa wameniambia pia niwe mwangalifu katika mavazi,
of-course ni kweli kitu kama hicho kinaweza kutokea kwahiyo sisi ni
binadamu, nimeshukuru sana kwasababu wameweza kunielewa, basi ni hivyo
tu nina furaha kwaajili ya hiyo kitu.” Alimaliza Shilole.
0 comments:
Chapisha Maoni