Supastaa wa Bongo Muvi, Vincent Kigosi, ‘Ray’ anateswa na tuhuma
anazopata kutokana na mtu asiyejulikana kufungua akaunti feki ya
Facebook yenye jina la Ray kisha kuposti picha za utupu.
Ray amesema kuwa japokuwa ametoa
ufafanuzi kupitia mtandao wake wa Instagram kuhusu picha hizo na akaunti
hiyo feki, anashangaa kuona watu wanamuandama na kukomalia kwamba yeye
anahusika.
“Yaani hii ishu inaniumiza na nimetoa ufafanuzi lakini sieleweki,
naomba niseme kwamba mimi ni mtu ambaye najiheshimu sana, siwezi kufanya
kitu kama kile mashabiki zangu waelewe hivyo tu,” alisema Ray.
0 comments:
Chapisha Maoni