test

Jumanne, 2 Juni 2015

AJALI MBAYA SANA: LORI LA MAFUTA LAUA WATU 70 PAPO HAPO>>.>SOMA HAPA


Lori lililopata ajali, hapa jitihada ya kuzima moto huo zikiendelea.
Takribani watu 70 wamefariki dunia huko mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto na kuteketea vibaya.
Police wanasema huenda kilichosababisha moto huo ni ajali.
Walioshuhudia wanasema dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti ndipo likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.
Mmoja ya waliokuwa wakishughulika kuwanusuru waliojeruhiwa amesema magari mengine 12 nayo yalishika moto.
Mwandishi wa BBC aliyeko Nigeria anasema mikasa ya ajali zinazohusu magari ya kubeba mafuta hutokea mara kwa mara nchini humo.

Miaka mitatu iliyopita ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliwaua watu Zaidi ya 100 huko Niger Delta katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.

NA BBC

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni