Mbunge wa jimbo la Vunjo, Augustino Mrema, ameonesha kukata tamaa
kutokana na kupewa tuhuma mbalimbali na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuhusiana na ubadhilifu wa fedha jambo ambalo ni kunyume na ukweli
uliopo.
Akichangia Bungeni mjini Dodoma, amesema kuwa anajua tuhuma hizo ni
kutokana na kutaka kumuangusha kisiasa ili kuweza kuchukua jimbo la Vunjo,
na kudai kuwa kamwe wananchi wake wa Vunjo, hawashawishiwi kiurahisi
kutokana na kuona juhudi zake katika kutafuta maendeleo.
Hizi ni sentensi alizoziongelea Mrema “Mimi pale Jimbo la Vunjo Shule
ya Muungano iliungua, nilitoa Mil.21 kwenye mfuko wangu wa Mbunge ili
kusaidia, mbona sioni Wizara mmetenga shilingi ngapi?”
“Mwisho akaja Katibu Mkuu wa CCM, na nyie CCM mmeanza kushiriki
katika uongo.. Katibu Mkuu badala ya kwenda kuwapa pole kwenye Jimbo
langu anasema ‘kila Jimbo lina mfuko wa Mbunge ambao ni Mil. 25 kwa
miezi mitatu, kwa mwaka ni Mil.100, hamuwezi kuwa na Kiongozi ambae ni
Mbunge na wakati huohuo ndie Mwenyekiti wa Mfuko huo, je si
atajipendelea?’.. Naomba niulize Serikali, ni kweli Vunjo tumepata Mil.
400 kama alivyosema Kinana au mnanipakazia?”
“Kwa nini mnakuja kwangu mnasema maneno ya uongo nyie CCM? Kwa nini
CCM mnanichangia kama mpira wa kona kule Vunjo? Kwa nini mnajiunga na
Wapinzani kwa kusema maneno ya uongo?”
“Mlizonipa ni Mil.150 lakini mnaenda Vunjo mnawaambia watu nimechukua
Mil. 400, naomba katika Mil. 400 mtoe hizo Mil.150 mnipe hiyo chenji
tena leo hii”
“Kwa nini mnaenda kusema hivyo jamani mna ajenda gani na mimi? Uongo
huu umenisononesha, na mimi nataka niwaambie CCM kwamba habadilishwi mtu
kule Vunjo. Hizi mbinu zinazotumika kunidhoofisha.. Nataka chenji yangu
nikafanye nayo Kampeni”
0 comments:
Chapisha Maoni