Kajala Masanja akionekana na jeraha
usoni kipindi ambacho alikua amepigwa chupa. Maskini Kajala! Ndivyo
unavyoweza kusema ukisikia mkasa wa staa wa kiwango cha juu kwenye
tasnia ya filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, ambaye anadaiwa kwa
hivi sasa hayuko sawa kiafya baada ya kupigwa chupa kichwani akiwa
katika shoo ya kumchangia mke wa msanii Mabeste iliyofanyika New Maisha
Club, Masaki jijini Dar.
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu
wa Kajala kimeliambia Ijumaa Wikiendakwamba, tangu staa huyo akumbwe na
sekeseke hilo amekuwa katika kipindi kigumu kwani amekuwa akipata
maumivu makali sehemu ya kichwani huku akianguka mara kwa mara.
Kajala Masanja. Kilidai kwamba, pia
Kajala amekuwa akipata kizunguzungu kikali hivyo kujiona yupo kwenye
hatari kubwa hasa ikitokea akaanguka vibaya kwani anaweza kupoteza
maisha.
0 comments:
Chapisha Maoni