SHIRIKA
la Maendeleo ya Petrol nchini, TPDC limeanza utafiti wakijiolojia wa
utafutaji mafuta na gesi katika vijiji vya Gombero mkoani Tanga.
Kutokana
na hilo shirika hilo limeanza kutekeleza mradi wa uchongaji wa mashimo
mafupi,visima vifupi kumi kwa ajili ya shughuli hiyo ya utafiti. Mradi
huo unafanywa na kumilikiwa TPDC kwa asilimia 100.
Akizindua
mradi huo Mgeologia, Amina Kagera alisema lengo kubwa la mradi huo ni
kuwapa mafunzo wataalam vijana wa TPDC kwa kuwatumia wataalam wa ndani
ya shirika waliobobea.
Alisema
fursa hiyo itawapa hamasa vijana kufanya tafiti mbalimbali nchini
lengo likiwa ni uendelezaji wa utafutaji wa mafuta na gesi kwa faida ya
watanzania wote.
"Mradi
huu ulianza rasmi mwaka 2010 ukiwa na malengo ya kuwajengea uwezo
wataalam wa sayansi ya utafutaji wa mafuta na gesi ambao hawakuwa na
msingi wa taaluma ya kijiolojia kama wale wa fani ya jiofizikia na
uhandisi"alisema Kagera
Kagera
alisema mradi huo unahusisha wataalam wa kukusanya sampuli za
jiolojia,jiokemikia na kuchambua sampuli, kufanya tafiti mbalimbali
kuhusisha sampuli hizo na utengenezaji wa ramani za kijiolojia katika
maeneo husika.
Alisema pia utaongeza thamani katika mabonde ya Tanzania ambapo shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi hufanyika.
"Mwaka
2012 hadi 2013 baada ya kazi za vitendo katika maeneo ya Kakindu na Mto
kibindo karibu na bwawa la Nairobi,Gombero Mkoani Tanga wataalam
waligundua uwepo mkubwa wa miamba tabaka aina ya Shalena,Silti Shale na
makaa ya mawe" alisema Kagera
Naye
Mkurugenzi wa Utafiti, Emma Msaky alisema malengo makuu ya mradi huo ni
kuzidi kuyaanisha maeneo ya utafutaji wa mafuta na gesi ili kujua uwepo
wa miamba ya uzalishaji wa nishati hizo.
Alizitaja
gharama za uchorongaji wa mashimo hayo na visima hivyo vifupi ni
takribani dola za Kimarekani 195,000 ambapo fedha zote hulipwa na TPDC
kutoka kwenye mfuko wake wa fedha za miradi ya maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni