MBUNGE
wa Ubungo John Mnyika amemshukia Waziri mkuu Mizengo Pinda na kumtaka
kuhakikisha kwamba kiasi cha fedha cha Bilioni tatu zitakazotolewa na
mfuko wa maafa zinatolewa kwa wakati ili kutatua changamoto za
waathirika.
Mbali
na hilo amemtaka Rais Kikwete pamoja na Waziri Pinda kumfuatilia Waziri
wa Ujenzi John Magufuli kwani alisema mfuko wa barabara umetoa milioni
10 kwa kila Manispaa lakini hadi kufikia sasa fedha hizo hazijaonekana.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mnyika alisema hatua
zote zitaweza kuongeza kasi zaidi endapo fedha hizo zitapatikana kwa
wakati.
Alisema
taarifa ya Waziri Pinda kuhusu maafa aliyosema ameipata haikuwa
inajitosheleza kwani yapo mambo ya msingi kwenye maeneo yaliyokubwa na
maafa hayakuzingatiwa.
“Taarifa
ya Waziri Pinda aliyosema ameipata kuhusu mafuriko haikuwa
imejitoshelaza na hili nililibaini baada ya kuzunguka katika Kata 12
kati ya 14 za jimbo la Ubungo,”alisema Mnyika.
Alisema kwa upande wa Jimbo wameshakaa kikao cha mfuko wa maendeleo na kutenga fedha kwa ajili ya maafa.
“Kikawaida
jimbo kwa mwaka linakusanya miliono 69 ambapo kati ya hizo asilimia 10
zitaenda kusaidia maeneo yaliyokubwa na maafa ikiwemo Mburahati kuzibua
mifereji iliyoziba ,”alisema Mnyika.
Hata
hivyo Mnyika aliendelea kusema kuwa katika kuhakikisha kwamba
miundombinu iliyoharibiwa na mvua inakarabatiwa upande wa barabara za
lami zilizoathirika iangalie wakandarasi wa kwenda kuziba sehemu
zilizoharibiwa.
Alisema
pia barabara za changarawe wazabuni na wahandisi waagizwe ili kufanya
tathimini katika maeno husika ili yaweze kukarabatiwa kwani wananchi
wanateseka sana.
Alisema
kwa upande wa manispaa ya Kinondoni wametenga kiasi cha Sh milino 10
ambazo zitatolewa kwa awamu kwa kila Kata ili ziweze kusaidia kuboresha
miundombinu ya barabara zilizoharibiwa kipindi cha mvua.
“Natambua
kwamba kuna baadhi ya wananchi kuanzia sasa wameanza kuchanga fedha ili
kuhakikisha kwamba wanaboresha mindombinu yao ikiwemo Kata ya Sinza ni
wakati wa kuunganisha nguvu za pamoja ili kuweza kufikia malengo,”alisema Mnyika.
Hata
hivyo alisema wakati akizunguka katika Kata 12 za Jimbo hilo alibaini
kuwa shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO) hawajaweka
wazi kwani wananchi hawapati maji kama ratiba ilivyopangwa hivyo
wamekuwa wakitegemea maji ya Mvua.
Kufuatia
hali hiyo aliitaka DAWASCO kuzunguka katika maeneo mbalimbali ili kuona
adha wanayopata wananchi na sio kukaa maofisini.
“Kitu
cha kuhoji ni kwamba kwanini Bomba la gesi kutoka Mtwara limekamilika
kwa wakati lakini miradi hii ya maji ambayo ipo ndani ya jiji la Dar es
Salaam haikamiliki kwa kipindi kinachotakiwa ?,”alihoji Mnyika.
Aidha
alisema Rais Jakata Kikwete bado hajatekeleza ahadi za wananchi kwani
wakati anazindua Daraja la Golani aliahidi Wananchi kuwa ataitisha kikao
kujadili masuala hayo na hakutekeleza hadi kufikia sasa.
Alisema
ili asije akaondoka na udhaifu huo ni vyema aitishe kikao hicho na yeye
ataendelea kubaki Dar es Salaam ili kujadili masuala hayo ya msingi.
“Ahadi
za Rais bado hazijatekelezwa wakati akitoa tamko linatekelezwa, lakini
tunaona fedha za ufisadi zinapatika ila za miradi ya maendeleo
hazipatikani,”alisema Mnyika kwa uchungu.
Alipoulizwa
kuhusu kugawanywa kwa majimbo alisema kuwa hakubaliani na hali hiyo
kutokana na kwamba inaiongezea gharama kwa Serikali.
Mbali
na hilo aliwataka wananchi kuhudhuria baraza la Madiwani Kinondoni leo
ambalo litakuwa linajadili suala hilo na waweze kutoa maoni yao.
0 comments:
Chapisha Maoni