Gerrard akiwapungia mkono mashabiki huku akiaga kwa kipigo
GOLI la dakika 26′ kipindi cha
kwanza la Adam Lallana liliashiria Liverpool watamuaga kwa furaha
nahodha wao Steven Gerrard ambaye amecheza mechi ya mwisho uwanja wa
Anfield dhidi ya Crstal Palace.
Lakini dakika ya 43′ katika
kipindi hicho Jason Puncheon alisawazisha goli hilo na kuinyamazisha
Anfield, huku kila shabiki akitafakari nini kitatokea katika siku hii
kubwa kwa nahodha na kiongozi wa Liverpool, Gerrard.
Liverpool wakihaha kutafuta
goli la kuongoza, Wilfried Zaha katika dakika ya 60′ akaifungia Palace
goli la pili sekunde 22 tu baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi.
Marudio ya video yameonesha kama Zaha alikuwa ameotea kabla ya kufunga, wewe unaonaje?
Dakika za lala salama, Palace
waliwasha moto mkali, dakika ya 90′ Glenn Murray alikosa penalti, lakini
katika dakika hiyo hiyo Glenn akamalizia mpira uliookolewa na kipa
Mignolet, hivyo kuandika goli la tatu.
Zaha akifunga goli la pili
0 comments:
Chapisha Maoni