Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
RAIS
Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa anatarajia kufungua mkutano wa Kanda ya
Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi
(OGP).
Taarifa
iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa kuwa
mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Utawala Bora
Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, mwaka huu
katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dhumuni
la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa masuala
mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili kutoa mrejesho kwa
wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.
“Kupata
uzoefu wa utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la
Afrika nan je ya Afrika kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha
uwajibikaji” ilieleza taarifa hiyo.
Mkutano
huo ni wa kwanza kufanyika nchini na wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo
kwa mara ya kwanza ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka 2013.
Mkutano
huo unatarajiwa kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za
kirai, Washirika wa Maendeleo wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya
nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali,
wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la Afrika.
Washiriki
wengine ni kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe
pamoja na washirika wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF,
UNESCO, MCC, USAID, DFID na JICA.
0 comments:
Chapisha Maoni