Skip to content
Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya
mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza kutumika rasmi
Hivi ni baadhi ya vipengele vilivyozua utata katika sheria hiyo
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa
kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu
akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).
2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za
siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla
(Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).
3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama
‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa
milioni 30; Sasa kama mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia
lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!
4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu
mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka
mmoja?
5. Rejea adhabu ya ibara mbalimbali: Sheria hii kila kosa linaweza fanya
mtu afungwe kifungo hadi cha maisha na kulipa pesa hadi zisizohesabika
kwani hakijawekwa kikomo cha juu cha adhabu bali kikomo cha chini tu kwa
Kiingereza “not less than”
6. Sheria haijaeleza vizuri suala la kutumia jina lisilo lako kwenye
mtandao na hivyo mtu anaweza kushitakiwa kama kuna mtu mwingine mwenye
jina kama hilo katika maisha halisi.
7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo
lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha. Kumbuka
hata ESCROW, EPA walisema ni uwongo; ni wangapi katika mtandao
wangeshtakiwa kiuonevu kwa hili?
8. Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha,
kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu
ya kuuboresha au kuufuta. Ni mara ngapi unafuta ‘status’ zako za
WhatsApp? Unaweza shtakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na
hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.
9. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe
umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au
hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya
Mahakama.
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni