test

Ijumaa, 15 Februari 2019

Nembo maalum ya mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) yazinduliwa...Mwakyembe Aifagilia


Nembo maalum ya mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) imezinduliwa leo  Alhamisi February 14  jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa nembo hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini chini ya Usimamizi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.


Mwakyembe ameipongeza Nembo hiyo  na kusema kuwa  imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangaza Tanzania hasa vivutio vya utalii.

"Nembo hii imebeba vitu vikubwa vitatu katika nchi yetu na mashindano haya. Kwanza imebeba dhana ya utalii. Kivutio chetu kikubwa cha Tanzania Kimataifa ni mlima Kilimanjaro. Tunauona hapa.

Lakini pili imebeba dhana ya uhifadhi. Tumeambiwa kuna pembe ya tembo na ya kifaru. Ambao ni wanyama wetu tunaowahifadhi kwa nguvu zetu zote. Tatu, yote haya yanahusu michezo na ndio maana kuna mpira," alisema Dk Mwakyembe.

Mkurugenzi wa masoko wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Aaron Nyanda alisema kuwa nembo hiyo imechorwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania.

"Tulianzisha mchakato kwa watu kubuni nembo ambayo tumeipata hii inayoonyesha vivutio vilivyopo hapa nchini. Na mshindi aliyeshinda atapata fursa ya kwenda nchini Peru ambako kutafanyika Fainali za Dunia kwa vijana wa umri huo iwapo tutafanikiwa kufuzu," alisema Nyanda.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni