Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma (CUF), ameitaka serikali kuwaua watu watakaokamatwa na madini ya Tanzanite.
Amesema
pamoja na serikali kuzungushia ukuta machimbo ya madini hayo Mirerani,
mkoani Arusha njia pekee ya kukabiliana na watoroshaji hao ni kuyaweka
katika orodha ya nyara za serikali ili watakaokamatwa nao wauawe.
Nachuma
ameyasema hayo jana Mei 31, bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akichangia
bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Lakini
pia serikali inunue mashine za kuchakata madini ya Tanzanite nchini
badala ya uchakataji huo kufanyika nje ya nchi ikiwamo India ambako
madini hayo yamesababisha ajira laki sita,” alisema.
Katika
hatua nyingine, Mbunge wa Viti Maalumu Catherine Magige aliitaka
serikali ifanye kila linalowezekana katika kudhibiti utoroshwaji wa
madini ya Tanzanite kwa kuwa bado yanatoroshwa nchini ijapokuwa kuna
ukuta umejengwa.
0 comments:
Chapisha Maoni