Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema hataonekana
katika majukwaa ya siasa kwa sababu yeye ameteuliwa kuwa mtendaji na
si mwanasiasa wa chama hicho hivyo atatekeleza yale tu yanayoamriwa
katika vikao vya Halmashauri Kuu.
Dk.
Bashiru amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kukabidhiwa ofisi na kutambulishwa kwa watendaji wa chama
hicho, na Katibu Mkuu mstaafu, Abdulrhaman Kinana katika Ofisi kuu za
chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
“Mimi
nimeteuliwa kuwa mtendaji wa chama kazi niliyopewa si ya jukwaaani, ni
marufuku kwa watendaji kujihusisha na siasa hivyo watu wasitarajie
kuniona katika majukwaa.
“Jukumu
langu kubwa ni kutekeleza maazimio ya vikao, kutoa taarifa pamoja na
kusimamia maagizo ya chama haya ni masuala ya mezani si ya jukwaani wapo
waliopewa dhamana ya kukaa katika majukwaa,” alisema Dk. Bashiru.
Aidha,
alisema atalipa kipaumbele suala la serikali kuhamia Dodoma ambapo
katika miaka iliyopita walishindwa, hivyo ataanzia hapo na kuhakikisha
wanafanikiwa na ataendelea pale walipoanzia.
0 comments:
Chapisha Maoni