Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Wizara imemwandikia barua Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ili kubadili sheria na kila mtu aweze kujipima Ukimwi
nyumbani.
Waziri
Ummy ameyasema hayo leo Mei 31 bungeni wakati akijibu swali la nyongeza
la Mbunge wa Mtambulie (CUF), Masoud Abdalla Salim ambaye ameuliza
mkakati wa ziada wa Serikali kutambua wanaopata athari za Ukimwi.
“Nchi
nyingine wanatumia mate kutambua waathirika wa VVU (Virusi vya Ukimwi),
Serikali ina mkakati gani wa ziada kutambua wale wanaopata athari za
VVU hasa tukianza na Mkoa wa Dodoma.”ameuliza Salim
Akijibu
swali hilo, Waziri Ummy ambaye pia ana dhamana ya maendeleo ya jamii,
jinsia, wazee na watoto amesema sheria imekuwa kikwazo kwa wananchi
kujipima maambukizi ya Ukimwi.
Waziri
Mwalimu amesema, ni kweli maambukizi yameongezeka kwa mkoa wa Dodoma
kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 5 sawa sawa na mkoa wa Tanga na
Mwanza.
“Tunafanya
utafiti maalumu kubaini kwa nini maambukizi yamepanda. Tumekuwa na
changamoto ya kuwapata wanaume kupima na njia ya mtu kujipima
mwenyewe,” amesema Waziri Mwalimu
Kuhusu dawa za VVU, Waziri Mwalimu amesema, zipo kwa asilimia 100.
“Ukimwi si sentensi ya kifo, ukibainika tunakuingiza katika mpango wa kupata dawa.” amesema
0 comments:
Chapisha Maoni