Waziri
wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Ndege ATCL Kapten Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa
Uendeshaji Kapten Sadick Muze kwa kosa la kumchagua rubani asiye na sifa
kwenda kupata mafunzo Canada.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Waziri Mbarawa amesema marubani watano
walichaguliwa kwenda nchini Canada kwa ajili ya kupata mafunzo ya
kurusha ndege mpya zitakazoingia nchini mwezi Septemba kama alivyoahidi
Rais Dkt. John Magufuli.
Waziri
ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa malipo ya awali ya ununuzi wa
ndege mbili mpya za shirika la ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu
Mkurugenzi huyo kuchagua marubani watano wenye sifa kwa ajili ya kwenda
kupata mafunzo nchini Canada ambapo kati ya watano waliochaguliwa mmoja
amebainika hana vigezo hivyo ameamua kuwasimamisha viongozi hao kutokana
na uzembe.
Aidha
waziri Mbarawa amewataka watendaji wa serikali kutimiza wajibu wao kwa
mujibu wa sheria na kanuni za kazi na mtumishi atakayefanya kinyume
hatasalimika kuwajibishwa.