Mwenyekiti
wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu,
amelitaka Shirika la nyumba la Taifa (NHC) kuacha tabia ya kuongeza kodi
mara kwa mara kwa wananchi ambao ni wapangaji katika nyumba hizo.
Zungu
amesema hayo jana Mei 30, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, baaada ya
kupitishwa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza
kuwa wapangaji katika nyumba hizo wengi ni maskini hawana uwezo wa
kulipa kodi zinazopanda kila kukicha.
“Mkurugenzi
wa shirika la nyumba, maagizo ya Waziri Mkuu umeyasikia, kaa na kamati
ya wapangaji, mimi shida kwangu ni nyumba ndiyo ajenda zangu za Ubunge
na Waziri Mkuu amesema muachane na haya mambo ya kupandisha kodi
kiholela, hawa ni watanzania hawana uwezo huo” alisema Zungu
Kwa
upande mwingine mwenyekiti huyo aliipongeza Wizara hiyo kwa kuleta
mabadiriko ya kiutendaji na kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.
Jana
Mei 30 2018, Bunge lilikubali kupitisha makadirio ya Bajeti ya Wizara
ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na
jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 73.07 imeidhinishwa
0 comments:
Chapisha Maoni