Spika
wa bunge wa zamani Pius Msekwa amesema kuwa kazi ya upinzani ni kukosoa
na kuisaidia serikali katika kufikia maendeleo kama Katiba
inavyoelekeza.
Msekwa
ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha East Africa BreakFast
kinachoruhwa na East Africa Radio kuwa utaratibu wa uendeshaji wa bunge
la vyama vingi umeainishwa kwenye kanuni za Bunge.
“Wakati
tunahama kutoka bunge la chama kimoja na kwenda bunge la vyama vingi
tuliandaa kanuni mpya kwa lengo la kuhakikisha upinzani utakapokuwa
bungeni utekeleze jukumu lake kikatiba ambalo ni kuikosoa serikali”
amesema Msekwa
Msekwa
ameongeza kuwa jukumu la upinzani haliishii kukosoa tu bali kuleta
mawazo mbadala pia ili kuisaidia serikali kuu katika kutimiza wajibu
wake.
0 comments:
Chapisha Maoni