Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
kuwa ataendelea kupaza sauti kupigania haki za wafanyakazi.
Zitto
ametumia mitandao yake ya kijamii kueleza hayo, ikiwa leo ni siku ya
wafanyakazi amewatakiwa Kila la kheri Wafanyakazi wote nchini huku
akiwataka kutimiza wajibu wa kuleta mabadiliko.
"Mei Mosi 2018: Kila la kheri Wafanyakazi wote nchini. Tutimize wajibu wa kuleta mabadiliko
"Licha
ya kwamba Wafanyakazi rasmi ni 9% tu ya nguvu kazi ya nchi yetu, ( kwa
kigezo cha Kodi ya Mapato ), Wafanyakazi kupitia PAYE wanachangia 75% ya
Kodi ya Mapato inayokusanywa na Serikali. Waajiri kupitia kodi za
makampuni ( taxes on incomes/interests, profits and capital gains )
huchangia 25% tu.
"Wafanyakazi
wanaumizwa na mzigo wa kodi kwa sababu hawana fursa za kukwepa kodi
kisheria maana kodi zao hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara
yao tofauti na wenye mitaji ambao huweza kukwepa kodi kwa mujibu wa
sheria.
"Tutaendelea
kupaza sauti kupigania haki za Wafanyakazi, kuhakikisha Uchumi
unazalisha ajira rasmi nyingi zaidi na mazingira ya Kazi kuboreka.
"Tunatuma
salaam za mshikamano kwa tabaka la Wafanyakazi nchini Katika siku hii
muhimu kwao. Wafanyakazi kwenye sekta rasmi wanaofikia 2.1 milioni ni
jeshi kubwa la kuleta mabadiliko nchini kwetu. Tutimize wajibu huo.
"Mapambano yanaendelea. Mshikamano daima.
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
1/5/2018
0 comments:
Chapisha Maoni