test

Alhamisi, 10 Mei 2018

Waziri Azitaja Kampuni 4 Zilizoruhusiwa Kuagiza Sukari Nje ya Nchi


Serikali imesema hali ya ukame uliozikumba nchi za ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika mwaka 2017/18 umesababisha Tanzania kushindwa kufikia matarajio ya sukari tani  314,000 na badala yake imezalisha tani 300,399.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji ya mwaka 2018/19, waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage amesema takwimu hizo ni za hadi kufikia Aprili 20, 2018.

Amesema mahitaji ya sukari nchini ni takribani tani 630,000 kwa mwaka na kwamba kati ya kiasi hicho tani 485,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani.

“Sukari kwa matumizi ya viwandani haizalishwi hapa nchini. Uwezo wa uzalishaji wa ndani kwa sasa ni wastani wa tani 320,000 kwa mwaka. Pengo la mahitaji takriban tani 165,000 za sukari ya kawaida na tani 145,000 za viwandani huzibwa kwa kuagizwa kutoka nje ya nchi,”amesema.

Amesema kampuni nne zinayozalisha sukari nchini ndizo zilizopewa jukumu la kuagiza sukari  kwa  masharti kuwa hakutakuwa na upungufu wa sukari nchini na ni lazima wapanue mashamba ya miwa ili ifikapo mwaka 2020  Tanzania ijitosheleze kwa sukari.

Amezitaja kampuni zilizopewa jukumu la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuwa ni Kilombero , TPC, Kagera na Mtibwa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni