Rais
John Magufuli ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Morogoro, kuweka
utaratibu mzuri ili wamachinga waweze kuuza bidhaa zao ndani ya stendi
ya mabasi ya Msamvu ya mjini Morogoro.
Kiongozi
mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 6, 2018 katika
uzinduzi wa stendi hiyo, kubainisha kuwa yeye ni Rais wa Watanzania
wote.
“Nimekuja
kufungua stendi lakini si kufungua stendi ambayo ina ubaguzi.
Nimechaguliwa na Watanzania wote. Niwaombe tu mtengeneze mkakati mpya
kuwawezesha wamachinga kuruhusiwa kuingia humu na wapewe vitambulisho,”
amesema.
Ametoa
kauli hiyo baada ya kuuliza iwapo wamachinga wanaruhusiwa kufanya
biashara katika stendi hiyo, kujibiwa na mamia ya waliofika kushuhudia
uzinduzi huo.
“Fedha
isiyojali maskini ni fedha haramu. Wito kwa waziri wa Tamisemi lazima
kuwe na eneo la kufanya biashara kwa wamachinga wote katika stendi
zitakazojengwa. Fedha zimnufaishe kila mmoja,” ameagiza Rais Magufuli na
kuongeza:
“Mnawanyima
nafasi wananchi wa hapa maana hawatauza mihogo, machungwa na bidhaa zao
kwa wasafiri wanaopita hapa. Ninawaomba manispaa kuangalia jambo hili…
lazima tutengeneze utaratibu mzuri utakaowanufaisha watu wote.”
0 comments:
Chapisha Maoni