Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa kwa siku kadhaa
zilizopita amekuwa katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa neno gani
anaweza kumpa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche kufuatia
kifo cha mdogo wake Suguta ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu na askari
Mbowe
amesema kuwa kifo ambacho kilimpata mdogo wake na Heche kinaumiza sana
ndiyo maana kwa siku kadhaa amekosa maneno mazuri ya faraja kumpa
kiongozi huyo wa CHADEMA
"Ni
siku ya 3 sasa toka ulimpozika mdogo wako, nimefikiria kwa muda mrefu,
maneno gani nitumie kukupa pole lakini imeniwia vigumu sana kuyapata
maneno hayo kutokana na aina ya kifo kilichokatisha maisha ya kijana
mdogo kabisa katika Taifa.
"Tunafundishwa
ya kwamba tushurukuru kwa yote,liwe baya au zuri, sawa tunashukuru
lakini kwa kifo cha aina ya mdogo wako kinauma na kuumiza sana, bora mtu
akiumwa inakuwa ni rahisi mnasema ni kazi yake Mungu hakuna anayeweza
kuipinga na huwa ni kipindi kigumu kuliko wakati mwingine wote wote
katika maisha yetu wanadamu pale tunapoondokewa na wapendwa wetu lakini
kwa kifo cha aina ya mdogo wako ni maumivu zaidi"
Aidha Mbowe alitumia wakati huo kutoa pole kwa familia ya John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake huyo
"Nakupa
pole sana Kamanda Heche John katika kipindi hiki kigumu, Mungu akupe
nguvu wewe, familia, ndugu, jamaa na marafiki, pole kwa mara nyingine
kamanda, apumzike kwa Amani Kamanda Suguta"
0 comments:
Chapisha Maoni