Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu alisema kwamba jengo la mahakama
hiyo na mali zote zilizokuwamo ndani, ziliteketea saa tatu usiku wa
kuamkia juzi.
‘Tulipata
taarifa kwamba mahakama inaungua tuliwataarifu wenzetu wa zimamoto,
lakini wote tulikuta jengo limeshateketea na nyaraka zote zikiwamo
pikipiki mbili ambazo zilikuwa ni kielelezo katika moja ya kesi,”
alisema Taibu na kuongeza:
“Baada
ya kukuta hali hiyo tulijiuliza maswali kadhaa imekuaje. Je, mahakama
ile ina walinzi, tukaambiwa inao, bahati mbaya walinzi hawakuwapo wakati
huo na hatujui walikwenda wapi?”
Alisema hawajajua chanzo cha tukio hilo hivyo jitihada zinaendelea ikiwamo kuwasaka walinzi hao.
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Moses Mwidete alisema hakuna
kilichookolewa kwa kuwa inaonyesha wakati moto huo unazuka hapakuwapo na
mtu yeyote, hivyo nyaraka zote muhimu ziliungua.
“Ulinzi
upo na ni walinzi wetu (mahakama), lakini hatujui kilichotokea kwa kuwa
mlinzi aliyekuwa zamu hatujui alipo hadi muda huu (jana mchana), kila
tukipiga simu yake inaita tu haipokelewi na muda mwingine anakata kabisa
simu,” alisema Mwidete na kuongeza:
“Tumeomba wenzetu wa polisi na watu wa mitandao watusaidie kupitia utaalamu wao wa kimtandao kumpata.”
Alisema
kazi ya kupata ukweli wa chanzo hicho unaendelea na kitengo cha ulinzi
na usalama kupitia ofisi ya kamanda wa polisi mkoa na Kikosi cha
Zimamoto na Uokoaji.
“Tumewaomba wenzetu wa zimamoto na polisi kutusaidia hili haraka iwezekanavyo.”


0 comments:
Chapisha Maoni