Rais
John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa Iringa pamoja na RPC
mkoani humo kumpatia msaada mwanamama Salmakoni Sanga ikiwa ni pamoja na
kumpima kama kweli ametolewa kizazi baada ya kudai kushambuliwa na
kijana aliyemtaja kwa jina la Mussa.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kumaliza kuhutubia katika sherehe
za Mei Mosi mkoani Iringa ambapo mama huyo alijitokeza na kumlilia Rais
Magufuli ampatie msaada kutokana na kunyimwa haki yake mahakamani.
Mama
huyo amesema kwamba tukio lake la kushambuliwa na Bw. Mussa lilifanyika
mwaka jana ambapo shambulio lilimfanya apoteze kiumbe kilichopo tumboni
hali iliyompelekea kutolewa kizazi.
Hata
hivyo mama huyo amesema kwamba pamoja na maumivu aliyosababishiwa na
kijana huyo, bado mahakama ilimuachia huru mtu huyo na yeye akiamini
kwamba alidhulumiwa haki yake na mahakama ya mkoa huo.
Akitoa
maagizo, Rais Magufuli amemtaka RPC Iringa Juma Bwire na Mkuu wa Mkoa
Bi. Amina Masenza kumtafuta kijana huyo na kumfungulia mashtaka upya
hata kama alishinda kesi.
0 comments:
Chapisha Maoni