Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa
juu ya wastani, kwa siku tano zinazoweza kusababisha mafuriko katika
maeneo mengi nchini .Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zitaanza leo
Mei Mosi mpaka Mei 5 mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha mikoa ya Dar es
Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mikoa mingine ni Mara, Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea katika jamii ni pamoja na adha ya usafiri, barabara kubwa kutopitika na maji kujaa au kupita kwa kasi.
Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.

0 comments:
Chapisha Maoni