Maofisa
watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini (Tanzania Investment Center
(TIC) wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Mei
22, 2018 maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.
Waliofariki
ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate
Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani
Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana amesema ajali hiyo imehusisha
gari ya serikali STK 5923 aina ya Toyota land cruiser lililongana na
Scania T620 AQV ambaye dereva wake alihama kwenye njia yake na
kusababisha ajali hiyo.
Waliopata
majeraha ni wawili Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari
hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus.
0 comments:
Chapisha Maoni