Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo ya
Ukanda wa Pwani kwani mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha kuanzia leo.
Taarifa ya TMA imesema maeneo yanayotarajiwa kupata mvua kubwa ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Utabiri
huo uliotolewa jana, Mei 11 umeonyesha kuwa kesho, Mei 13 kutakuwa na
ongezeko la mvua maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini.
0 comments:
Chapisha Maoni