Rais John Magufuli amezindua daraja la mto Kilombero ambalo kwa sasa linaitwa daraja la Magufuli.
Akitangaza
jina la daraja hilo leo Mei 5 wakati Rais akizindua, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ametoa jina hilo
kutokana na juhudi alizozifanya Rais Magufuli wakati akiwa waziri wa
ujenzi.
"Mheshimiwa
Rais kwa mamlaka niliyopewa natangaza rasmi daraja hili litaitwa
Magufuli, hii ni kutokana na juhudi kubwa uliyoiweka katika kufanikisha
ujenzi wa daraja hili," amesema.
Daraja hilo lenye urefu wa zaidi ya mita 300 linaunganisha wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.
0 comments:
Chapisha Maoni