WASANII
na watu mbali mbali wenye ukaribu na tasni ya burudani wameendelea
kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald
‘Masogange’, Zari The Boss Lady naye hajakaa kimya.
Zari
ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi
akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana.
Kupitia mtandao wa Snapchat Zari ameandika;
"We
were not friends as such but ever since you got my number you’ve been
dropping me a text every month and i mean no month passed without you
asking how are the kids. in peace sis."
Kwa kiswahili;
“Hatukuwa
marafiki sana lakini tangu upate namba yangu umekua ukinitumia meseji
kila mwezi na hakuna mwezi uliopita haujauliza kuhusiana na watoto
wanaendeleaje pumzika kwa amani dada”
Masogange
enzi za uhai wake aliweza kutokea kwenye video za wasanii kama AY na
Mwana FA, Belle 9, Tunda Man, Izzo Bizness na wengineo.
Amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.



0 comments:
Chapisha Maoni