Video
queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa
kuzikwa nyumbani kwao Wilayani Mbozi, mkoani Mbeya ambako ndiko wazazi
wake waliko.
Dada
wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes utaagwa
jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni siku ya
kesho Jumapili kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Ambapo
misa itafanyika viwanjani hapo kisha kuanza safari rasmi kuelekea
Mbalizi mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa marehemu Agnes
Gerald mahali pema peponi.
“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.
Aidha imeelezwa kuwa kutakuwa na mabasi mawili yatakayobeba wasindikizaji wa mwili huo mpaka mkoani Mbeya.
Agnes
Masogange amefariki jana Aprili 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma
baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo
la pumu.


0 comments:
Chapisha Maoni