Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema wanaume wote
waliokaidi wito wa kufika ofsini kwake baada ya kupigiwa simu na
kutumiwa barua za wito watakamatwa na Jeshi la Polisi kuanzia siku ya
jumatatu ya April 23.
RC
Makonda amesema ifikapo siku ya Jumapili majina ya wanaume waliokaidi
wito yatafikishwa kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam
Lazaro Benedict Mambosasa kwaajili ya utekelezaji.
Aidha
RC Makonda ameongeza siku nyingine tano kwaajili ya kusikiliza kesi
zilizowasilishwa ofisini kwake na kufanya idadi ya kufikia siku 15.
Pamoja
na hayo RC Makonda amesema ataunda kamati ya wanasheria na maafisa
ustawi wa jamii kutoka serikalini na taasisi binafsi kwaajili ya kufanya
uchambuzi wa ukubwa wa tatizo na mapendekezo ya kisheria kisha
kuwasilishwa wizara husika kisha kuwasilishwa Bungeni.
Hata
hivyo RC Makonda amesema ifikapo April 25 na 26 atatoa ripoti ya
mwelekeo dhidi ya mateso waliyokuwa wakipata kinamama na watoto
waliotelwkezwa.
RC
Makonda amesema Zoezi la kusikiliza kinamama waliotelekezwa limekuwa na
mafanikio makubwa ambapo zaidi ya wananchi 17,000 walifika ofsini kwake
ambapo hadi sasa kinamama 7,000 wamesikilizwa na wanaume 1,200
wamekubali kwa maandishi kutunza watoto wao na wengine wamepimwa DNA.


0 comments:
Chapisha Maoni