Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji wa madini nchini kuondoa
hofu ya kukosa haki zao kwani kamati ya pili iliyoagizwa kufanya
uchunguzi kuhusu mchanga wa madini (makinikia) bado haijakamilisha kazi
yake.
Waziri
Mkuu alisema hayo jana wakati akijibu swali la mbunge wa Tabora Mjini,
Emmanuel Mwakasaka, lililohoji kuhusu taswira ya Tanzania kimataifa hasa
katika uwekezaji wa madini.
Majaliwa
aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa kamati ya pili
iliyoundwa kuangalia athari za kisheria, kisiasa na kimataifa kuhusu
sakata la mchanga wa madini bado haijatoa ripoti yake.
“Watanzania
wengi walikuwa na hofu, hata wabunge wengi katika serikali hii ya awamu
ya tano mmekuwa mkizungumzia sakata la mchanga wa madini, lakini
niwatoe hofu, Rais John Magufuli alifanya hayo kwa nia njema ya kulinda
rasilimali za Taifa,” amliema
Waziri
Mkuu aliwataka wawekezaji wa madini kuondoa hofu kwa kuwa serikali
itazingatia ushauri kutoka sekta nyingine kabla ya kuchukua hatua
katika sakata hilo la mchanga wa madini.
0 comments:
Chapisha Maoni