Muigizaji
wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka
na kusema kuwa Salma Jabu maarufu kama Nisha Bebe hana vigezo vya
kutembea na Ex boyfriend wake Brown.
Wiki
iliyopita picha za Nisha na Brown zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii
zikiwaonyesha wakiwa wanakumbatiana na hata kubusiana jambo lililozua
maneno huku ikisemekana kuwa ni wapenzi.
Lakini
mwishowe Nisha aliachia wimbo wake wa Bachela ambapo ilionekana kuwa
Brown alikuwa ni video king Kwenye video hiyo na wawili hao baadae
walikana tetesi zozote za Mahusiano ya kimapenzi wakidai ilikuwa ni kazi
tu.
Hatimaye
Wolper amefunguka kuhusiana na Mahusiano hayo na kuweka wazi kuwa
haamini kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Global Publishers Wolper amedai kuwa Nisha ni
mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo
huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown
haifanani kabisa na Nisha.


0 comments:
Chapisha Maoni